Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde amefungua rasmi maonesho ya Wiki ya Ushirika Duniani kitaifa katika Manispaa ya Tabora. Maadhimisho ya Wiki ya Ushirika Duniani kitaifa yanafanyikakwenye viwanja vya Nanenane Ipuli Manispaa ya Tabora mkoani Tabora.Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 1 Julai, 2023 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.