Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe amefungua kikao cha Wadau wa Kilimo kilichoandaliwa na kuratibiwa na Taasisi ya African Agriculture Transfomation Initiative (AATI).
Aidha Mhe. Bashe amefanya ufunguzi wa ofisi ya mageuzi ya kilimo yaani Agricultural Transformation Ofice ambayo itakuwa na jukumu la kuweka mpango mkuu wa wa nchi wa mageuzi kwenye sekta ya kilomo (Agriculture Transformation Master Plan) ambayo itakuwa muongozo wa mwelekeo wa sekta ya kilimo nchini.
Wakati wa ufunguzi huo Mhe. Bashe amesisitiza fikra za kuwahusisha vijana na wanawake kwa sera bora na teknolojia za kisasa ili kuvutia kundi lavijana kushiri kwenye sekta ya kilimo